Idadi ya wakimbizi wa Syria walioandikishwa mataifa jirani yaongezeka mara tatu zaidi

2 Oktoba 2012

Idadi ya raia wa Syria walioandikishwa au wanaosubiri kuandikishwa kama wakimbizi nchini Jordan , Lebanon, Uturuki na Iraq sasa imepita watu 300,000 ikiwa ni mara tatu zaidi ya idadi iliyoandikishwa miezi mitatu iliyopita. Takwimu za hivi majuzi zinaonyesha kuwepo kwa wakimbizi 311,500 kutoka Syria kwenye nchi hizo nne ikilinganishwa na wakimbizi 100,000 walioandikishwa mwezi Juni.

Kuendelea kuongezeka kwa kasi kwa idadi ya wakimbizi kunajiri juma moja baada ya shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa kutoa ombi la dola milioni 487 kusaidia wakimbizi 710,000 walio nchi majirani ifikapo mwishoni mwa mwaka huu. Pia familia zinazowapa mahitaji wakimbizi hao zinaripotiwa kupungukiwa na mahitaji. Adrian Edwards ni msemaji wa UNHCR.

(SAUTI YA ADRIAN EDWARDS)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud