Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania itaendelea kusaidia kusuluhisha mizozo kwa njia ya amani, asema Waziri Membe kwenye Umoja wa Mataifa

Tanzania itaendelea kusaidia kusuluhisha mizozo kwa njia ya amani, asema Waziri Membe kwenye Umoja wa Mataifa

Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania, Mwana Bernard Kamillius Membe, amezungumza kwa kirefu kuhusu desturi ya kusuluhisha mizozo kwa njia ya amani kwenye hotuba aliyoisoma kwenye mkutano wa 67 wa Baraza Kuu la UMoja wa Mataifa, ambako alimwakilisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Baada ya hotuba yake, Redio ya Umoja wa Mataifa ilipata fursa ya kufanya naye Waziri Membe mahojiano, ambako amezungumzia mambo mseto, yakiwemo kuzuia mizozo, usalama na maendeleo ya maendeleo ya milenia. Joshua Mmali alimuuliza kwanza Waziri Membe, ni ujumbe gani alokuja nao kwenye Umoja wa Mataifa kutoka kwa serikali ya Tanzania mwaka huu.

(Audio: 12.45)