Ban akutana na rais Sein wa Myanmar

29 Septemba 2012

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amekutana na rais wa Myanmar Thein Sein Jumamosi asubuhi.Katika mkutano huo, viongozi hao wawili wamebadilishana mawazo kuhusu mabadiliko ya kisiasa nchini Myanmar, pamoja na maendeleo ya kiuchumi na kijamii, na maridhiano ya kitaifa.

Wamejadili pia machafuko yaliyozuka hivi karibuni kwenye jimbo la Rakhine, pamoja na hatua za sasa na za muda mrefu za kuendeleza amani na utulivu, pamoja na jinsi ya kukabiliana na chanzo cha migogoro, zikiwemo juhudi za maendeleo. Rais Sein alithibitisha kuwa nchi yake itazingatia hatma ya baadaye ya suala hilo.

Bwana Ban amemsifu rais Sein kwa uongozi wake wa busara, na kumpa moyo aendelee kuzingatia harakati za kufanya mabadiliko, ambazo amesema Umoja wa Mataifa utaendelea kuunga mkono, na kuoa wito zifanywe juhudi zaidi kuishughulikia hali kwenye jimbo la Kachin

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter