Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ufadhili zaidi wahitajika kwa wakimbizi wa ndani Syria: UNICEF

Ufadhili zaidi wahitajika kwa wakimbizi wa ndani Syria: UNICEF

Shirika la Kuhudumia Watoto katika Umoja wa Mataifa, UNICEF, limesema kuwa ukaguzi wake wa hivi karibuni unaonyesha kuwa zaidi ya watoto 150, 000 ni miongoni mwa idadi kubwa ya wakimbizi wa ndani kwenye jimbo la Tartous mashariki mwa Syria, yapata mwendo wa kilomita mia kutoka mji wa Homs. Hadi sasa ni familia 12, 000 ambazo zimeandikishwa, ingawa gavana wa jimbo hilo anakadiria kuwa idadi kamili ni hadi familia 60, 000, zenye jumla ya watu laki tatu kwa pamoja.

Shirika la UNICEF limesema takriban watoto 20,000 waliohama makwao wanakwenda shule, na hakuna shule inayokaliwa na wakimbizi wa ndani katika eneoo hilo. Wengi wa wakimbizi wa ndani katika eneo hilo walitoka Homs na Hama, na wengine wamewasili kutoka mji wa Aleppo.

Mashirika ya kibinadam yaliyopo mji wa Aleppo yanasema mahitaji ni makubwa mno, na ingawa wakimbizi hawa wamepata usaidizi wa kibinadam miezi iliyopita, ufadhili wa misaada hii umepungua. Shirika la UNICEF limesema kuwa linajitahidi kuhakikisha mapengo yoyote ya utoaji misaada kutokana na uhaba wa fedha yanazibwa. Marixie Mercado ni msemaji wa UNICEF.

(SAUTI YA MARIXIE MERCADO)