Rais wa Equatorial Guinea ahimiza uungwaji mkono kwa nchi maskini

28 Septemba 2012

Rais wa Equatorial Guinea, Teodoro Obiang Nguema Mbasogo ameuambia mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa haja ya nchi maskini kupigwa jeki ili kuzikabili changamoto za kimaendeleo ikiwemo kutokomeza tatizo sugu la umskini.

Rais huyo amesema kiwango cha watu waangamia na matizo ya njaa katika nchi zinazoendelea kinazidi kile kinachoweza kujitokeza kwenye maeneo ambayo kunajitokeza mashambulizi ya kijeshi.

Ametaja mikwamo mingine inayoziandama nchi zinazoendelea ni pamoja kuongezeka kwa watu wasiojua kusoma na kuandika,kukosakana kwa makazi ya kudumu na matatizo ya utapiamlo .

Kiongozi huyo ametaka Umoja wa Mataifa kuanzisha mpango maalumu kwa ajili ya nchi maskini ili hatimaye zifaulu kuendesha ujenzi wa miundo mbinu itakayosaidia kusuma mbele shughuli za maendeleo.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter