Palestina sasa yataka haki ya taifa lakini isiyo mwanachama wa UM

28 Septemba 2012

Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas ambaye ombi lake la kutaka taifa lake kuwa mwanachama wa Umoja wa Mataifa liligonga mwamba mwaka uliopita sasa ametangaza azimio jipya la kutaka kuwa taifa huru lakini lisilo mwanachama wa Umoja huo.

Hata hivyo ameishutumu waziwazi Israel juu ya kile alichokiita kuendesha mipango ya kuibisha Palestina kwenye duru za kimataifa.

Akizungumza kwenye baraza la Umoja wa Mataifa Abbas amesema kuwa harakati ya Palestina siyo kufuta taifa lililoko tayari yaani Israel bali ni kujenga misingi ambayo kila mmoja atatambua kuwepo kwa taifa lijulikanalo Palestina.

Katika hotuba yake hiyo Kiongozi huyo pia alikosoa mwenendo wa jirani yake Israel ambaye alimtuhumu kuendesha mashambulizi yaliyowalenga raia.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter