Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yatoa huduma dhidi ya mkurupuko wa Hepatitis E kwenye kambi ya Dadaab

UNHCR yatoa huduma dhidi ya mkurupuko wa Hepatitis E kwenye kambi ya Dadaab

Kutokana na kuwepo dalili za mkurupuko wa ugonjwa wa hepatitis E kwenye kambi ya wakimbizi ya Dadaab kaskazini mwa Kenya , shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linaendesha hudumu za afya kwa umma zinazolenga kuboresha usafi kambini. Kambi ya Dadaab ina wakimbizi 473,000 na ndiyo kambi kubwa zaidi ya wakimbizi duniani.

Juma lililopita visa 223 vya ugonjwa huo viliripotiwa kwenye kambi tano za Dadaab huku pia vifo vya watu wanne ambao wote ni wanawake waliokuwa wamejifungua vikiripotiwa. Asilimia kubwa ya visa vya ugonjwa huo vimeripotiwa kwenye kambi ambazo hamna choo za kutosha na miongoni mwa wakimbizi wanaowasili sasa wasiodumisha usafi. Andrej Mahecic ni msemaji wa UNHCR.

(SAUTI YA ANDREJ MAHECIC)