Ban ahimiza ushirikiano wa kimataifa kutokomeza ugonjwa wa kupooza

27 Septemba 2012

Ulimwengu unatakiwa kushirikiana na Nigeria, Pakistan na Afghanistan ili kuutokomeza ugonjwa wa kupooza, au polio. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon siku ya Alhamis kwenye mkutano maalum kuhusu ugonjwa wa polio. Nchi hizo tatu ndizo ambazo bado zina visa vya maambukizi ya ugonjwa huo wa kulemaza viungo vya mwili miongoni mwa watoto hasa chini ya miaka mitano.

Bwana Ban amesema, watoto wakilindwa kutokana na ugonjwa wa kupooza, wanakuwa salama dhidi ya magonjwa yote. Na ili kupata ufanisi wa kote duniani, unahitajika ushirikiano wa kimataifa. Amesema kuwa hiyo ndiyo maana ameweka nguvu za mfumo wote wa Umoja wa Mataifa kwenye juhudi za kuutokomeza ugonjwa wa kupooza.

Visa vya maambukizi ya uogonjwa wa kupooza kote ulimwenguni vimeshuka kwa zaidi ya asilimia 99 tangu mwaka 1988, kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, WHO.

Ugonjwa huo wa kupooza hatuna tiba, lakini unaweza kuzuiwa kwa njia ya chanjo kwa watoto chini ya miaka mitano.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter