Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wazindua mkakati wa kusaidia mchango wa wanawake vijijini katika kuhakikisha usalama wa chakula

UM wazindua mkakati wa kusaidia mchango wa wanawake vijijini katika kuhakikisha usalama wa chakula

Mashirika manne ya Umoja wa Mataifa yameungana ili kuwapa uwezo vijijini kupitia mpango unaoendeleza ushirikiano wa kiuchumi na usalama wa chakula.

Wanawake wanawakilisha asilimia 70 ya wafanyakazi katika sekta ya kilimo katika baadhi ya mataifa, na mpango huo wa miaka mitano unalenga kuongeza ujira wao na kuendeleza kuhusika kwao katika taasisi za mikoani, pamoja na uongozi.

Mpango huo ni mchakato wa kitengo cha wanawakwe katika Umoja wa Mataifa, UN Women, na mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa yanayoshughulika na masuala ya chakula na kilimo, yakiwemo FAO, WFP na IFAD.

Mpango huo utazinduliwa kwanza katika nchi saba, zikiwemo Ethiopia, Guatemala, Kyrgyzstan, Liberia, Nepal, Niger na Rwanda. Mkurugenzi Mkuu wa UN Women Michelle Bachelet, amesema usalama wa chakula unaweza kuimarishwa, wanawake wakiweza kudai haki zao na kuweza kutumia ardhi.