Baraza la Usalama lapongeza utendaji wa Muungano wa nchi za Kiarabu

27 Septemba 2012

Baraza la Usalama limesema kuwa linafurahia mashirikiano mema yanayoendelea kuchipua baina ya Umoja wa Mataifa na muungano wa nchi za kiarabu  katika wakati ambapo kukishuhudiwa mageuzi mengi yakijitokeza katika eneo la Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini.

Baraza hilo la Usalama pia limekaribisha juhudi zinazochukuliwa na muungano wa nchi za kiarabu inayoendesha usuluhishi wa utanzuaji mkwamo wa Mashariki ya Kati kwa kuanzisha majadiliano yenye nia ya kuutatua mzozo katika eneo hilo kwa njia ya amani na upatanishi.

Kwa mujibu wa waziri wa mashauri ya kigeni wa Ujerumani Guido Westerwelle ambaye nchi yake inashika wadhifa wa rais wa baraza hilo, Jumuiya ya nchi za kiarabu imetoa mchango mkubwa kwa mashiriki ya Umoja wa Mataifa ukiwemo pia kusaidia vikosi vya ulinzi wa amani katika maeneo yaliyokumbwa na machafuko.

Nchi wanachama wa jumuiya hiyo kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa zilifaulu kutuliza hali ya mambo katika nchi za Tunisia na Libya wakati wa mageuezi ya kisasa yaliyozunguka eneo la Afrika ya Kaskazini.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter