Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Raia wa Nepal ashinda tuzo ya Wangari Maathai ya kulinda misitu

Raia wa Nepal ashinda tuzo ya Wangari Maathai ya kulinda misitu

Tuzo ya kwanza ya Wangari Maathai imemwendea mwanaharakati wa kulinda misitu kutoka taifa la Nepal, katika kutambua juhudi zake za kuendeleza udhibiti wa misitu wa kijamii.

Tuzo hiyo imetolewa kwenye hafla ya Kamati ya Misitu (COFO), katika makao makuu ya Shirika la Chakula na Kilimo, FAO mjini Roma.

Tuzo ya Wangari Maathai ilianzishwa na Ushirika wa Kimataifa kuhusu Misitu (CPF), ili kutambua juhudi za kuboresha na kuendeleza misitu, kwa heshima na kumbukumbu ya Wangari Maathai, ambaye alikuwa mwanaharakati wa mazingira kutoka Kenya, na mwanamke wa kwanza wa Afrika kuwahi kushinda tuzo ya amani ya Nobel kwa ajili ya mchango wake kwa maendeleo endelevu, demokrasia na amani.