Hakuna muda wa kupoteza kuleta demokrasia nchini Somalia:Ban

27 Septemba 2012

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelipongeza taifa la Somalia kutokana na jitihada ambazo limepiga kwenye mabadiliko ya kisiasa na kutoa wito kwa jamii ya kimataifa kuendelea kuliunga mkono taifa hilo la pembe ya Afrika akisisitiza kuwa hakuna muda wa kupoteza kwa kuwa taifa hilo bado linakabiliwa na changamoto za kibinadamu na za kiusalama.

Akiongea wakati wa mkutano mdogo kuhusu Somalia ulioandaliwa mjini New York kando mwa mkutano wa 67 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Ban amesema kuwa mabadiliko yaliyokuwa yakisubiriwa kwa muda yamewadia. Joshua Mmali na taarifa kamili.

(SAUTI YA JOSHUA MMALI)

Akizungumza na Radio ya Umoja wa Mataifa leo mjini New York, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu na Umoja wa Mataifa kuhusu Somalia, Augustine Mahiga, amesema kwamba Somalia imeingia kipindi kipya katika harakati za kurejesha amani na maendeleo ya kisiasa.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter