Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu umaskini na haki za binadamu kuizuru Namibia

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu umaskini na haki za binadamu kuizuru Namibia

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu umaskini na haki za binadamu Magdalena Sepúlveda anatarajiwa kufanya ziara rasmi nchini Namibia kuanzia tarehe 1 hadi tarehe 8 mwezi Oktoba mwaka huu kwa lengo la kupata habari kuhusu hali ya watu wanaoishi kwenye hali mbaya ya umaskini na hatua zilizochukuliwa na serikali kuboresha maisha yao na kuwahakikishia haki zao za binadamu.

Hata kama Namibia linaorodheshwa kama la kipato cha wastani lina viwango vya chini vya ugavi wa utajiri duniani. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)