Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM watoa ombi la dola milioni 487.9 kusaidia wakimbizi wa Syria

UM watoa ombi la dola milioni 487.9 kusaidia wakimbizi wa Syria

Umoja wa Mataifa unasema kuwa utahitaji karibu dola milioni 500 ili kuweza kushughulikia suala la wakimbizi nchini Syria zikiwa ni dola milioni 200 zaidi ya ombi lililotolewa mapema mwaka huu. Mashirika ya kutoa misaada yanakadiria kuwa idadi ya wakimbizi nchini Jordan, Lebanon,Iraq na Uturuki itaongezeka kutoka idadi ya sasa ya wakimbizi 300,000 hadi zaidi ya wakimbizi 700,000 ifikapo mwishoni mwa mwaka huu. Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa hadi wakimbizi 3000 kutoka Syria wanavuka mpaka na kuingia nchini majirani kila siku. Mashirika ya kutoa misadsa yanasema kuwa ufadhili zaidi unahitajika ili kujiandaa kwa msimu wa baridi unaokuja. Panos Moumtziz ni mratibu wa masusla ya wakimbizi wa Syria.

(SAUTI YA PANOS MOUMTZIZ)