Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utapia mlo ni tatizo kubwa kwa watoto nchini Yemen:WFP

Utapia mlo ni tatizo kubwa kwa watoto nchini Yemen:WFP

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, limesema kuwa utapia mlo ni tatizo kubwa miongoni mwa watoto nchini Yemen, ukiathiri takriban watoto milioni mbili mara kwa mara, ambayo ni karibu nusu ya idadi nzima ya watoto chini ya miaka mitano. Watoto wengine milioni moja wana utapia mlo wa kupindukia.

Shirika la WFP limesema kuwa taifa la Yemen ndilo la tatu kuwa na idadi kubwa zaidi ya utapia mlo duniani. Ingawa shirika hilo linajitahidi kutoa vyakula vyenye lishe kwa akina mama wazazi na watoto, linakabiliwa na kasoro ya takriban milioni 70 za fedha za ufadhili kwa ajili ya bejeti yake mwaka huu.