Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi wa Afrika watoa wito wa mwitikio wa kasi kwa ajili ya HIV/AIDS

Viongozi wa Afrika watoa wito wa mwitikio wa kasi kwa ajili ya HIV/AIDS

Viongozi wa Afrika wanaokutana katika kikao cha 67 cha Baraza kuu la UM, wametoa wito ufanywe ufumbuzi na ubunifu wa kuharakisha juhudi za kukabiliana na UKIMWI, kifua kikuu na malaria, na kuendeleza afya njema kwa watu wa bara hilo.

Katika mkutano wao uliokuwa makao makuu ya UM, viongozi hao wamejadili mkakati wa Umoja wa Afrika (AU) ambao unatoa mapendekezo ya mikakati endelevu ya fedha na kutoa huduma za kutibu na kuzuia HIV, pamoja na huduma nyingine za afya katika bara la Afrika ambalo ni moja kati ya malengo ya maendeleo ya Milenia (MDG’s).

Malengo haya yalikubaliwa na viongozi wa dunia katika mkutano wa kilele wa UM wa mwaka 2000 na kuweka malengo maalum ya HIV/AIDS, pamoja na kupunguza umaskini, elimu, usawa wa kijinsia, afya ya mtoto na uzazi, mazingira safi, na Ushirikiano wa maendeleo ya kimataifa. Shabaha ya kufikia malengo hayo ni mwaka 2015.