Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa mawaziri wataja umihumu wa ECOSOC kwenye maendelo duniani

Mkutano wa mawaziri wataja umihumu wa ECOSOC kwenye maendelo duniani

Mawaziri wa serikali na maafisa wengine wa ngazi za juu kutoka sehemu mbali mbali za dunia wamekusanyika mjini New York ambapo wameunga mkono baraza la kijamii na kiuchumi la Umoja wa Mataifa ECOSOC katika kuweka mikakata ya kukabiliana na changamoto za maendeleo endelevu duniani.

Wakati wa kufunguliwa kwa kikao maalum katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amesema kuwa baraza hilo la kiuchumi na kijamii linataoa mchango muhimu katika kutaua tatizo la ajira duniani na kuzuia hali mbaya ya kiuchumi kujirudia tena. Ban amesema kuwa nchi wafadhili zinastahili kujitolea kusaidia nchi zinazoendelea kutimiza malengo ya maendelo ya mileni kwa kupunguza umaskini na changamoto zingine duniani ifikapo mwaka 2015 na kuweka usalama wa chakula kuwa ajenda kuu.