Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushirikiano unahitajika kuendeleza hatua zilizopigwa kupunguza vifo vya mama wazazi na watoto:UM

Ushirikiano unahitajika kuendeleza hatua zilizopigwa kupunguza vifo vya mama wazazi na watoto:UM

Kumekuwa na hatua za kufurahia katika nchi nyingi, za kupunguza idadi ya vifo vya akina mama wazazi na watoto katika mwongo mmoja uliopita, imesema ripoti mpya ya wataalam huru.

Kundi hilo la wataalam lililoteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon liliundwa mnamo mwaka 2011, na lina jukumu la kukagua hatua zilizopigwa katika kuboresha afya ya akina mama na watoto, kutambua changamoto zilizopo, na kufanya mapendekezo. Hata hivyo, kwa sababu ya kupungua viwango vya ufadhili na kushindwa kuzilenga nchi zenye mahitaji makubwa zaidi, malengo ya afya duniani ambayo yanahusiana hususan na wanawake huenda yasifikiwe ifikapo mwaka 2015.

Joy Phumaphi, mtaalam mmoja kwenye kundi hilo, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Muungano wa Viongozi wa Afrika kuhusu Malaria, ametoa wito kwa nchi na wafadhili kuendeleza kasi ya hatua zilizopigwa

(SAUTI YA ....)