Afrika inastahili kuwa na mashirikiano yenye usawa na dunia:Rais wa Senegal

26 Septemba 2012

Rais wa Senegal Macky Sall amewaambia viongozi wa dunia kuwa njia pekee itayoweza kulivusha bara la afrika, ni kuhakikisha kuwa bara hilo linakuwa na mashirikiano yenye usawa na upande mwingine wa dunia.

Akizungumza kwenye kikao cha baraza kuu la Umoja wa Mataifa Sall amesema kuwa Afrika inaweza kupiga hatua kimaendeleo na kuimarisha mifumo yake ya kidemokrasia kama itapewa fursa sawa ya mashirikiano na jumuiya ya kimataifa.

Amesema vipaumbele vya afrika vinapaswa kutazamwa upya ili kushagihisha fursa za uwekezaji na kubadili msimamo wa mataifa makubwa kuhusu afrika,kutasaidia kulisukuma mbele bara hilo.

Rais Sall amesisitiza kuwa bara la afrika ambalo limepitia kwenye vipindi vigumu vya unyonyaji na biashara ya utumwa, kama haliko tayari kushuhudia likigeuzwa kama shamba la bibi kwa ajili ya kuwanufaisha wachache huku watu wake wakiendelea kuteseka na maisha.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter