Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua zapigwa Sudan lakini kuna changamoto kubwa upande wa haki za binadamu:Baderin

Hatua zapigwa Sudan lakini kuna changamoto kubwa upande wa haki za binadamu:Baderin

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya haki za binadamu Mashood A. Baderin amesema kuwa serikali ya Sudan imejitolea kutekeleza haki za binadamu na pia kuboresha hali ya haki za binadamu nchini humo. Hata kama hatua zimepigwa baadhi ya haki za binadamu bado hizijashulikiwa ipasavyo. Hali katika majimbo ya Darfur, Kordofan kusini na Blue Nile zinahitaji hatua za dharura hasa kwa wakimbizi wa ndani . Mjumbe huyo pia amezungumzia kuzuiwa kwa mashirika ya umma na kutokana hofu ya kushikwa hayawezi kutekeleza wajibu wao wa kutetea haki za binadamu.

Sudan inasema kuwa mtaalamu huyo amefanikiwa kukutana na mafisa wa serikali na wanachama wa mashirika ya umma wakati wa ziara yake na kusema kuwa hatua zimepigwa.