Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pillay ataka hatua kuwalinda mawakili, waandishi wa habari na wanaharakati wa haki za binadamu

Pillay ataka hatua kuwalinda mawakili, waandishi wa habari na wanaharakati wa haki za binadamu

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa, Navi Pillay, amesema kuwa mauaji ya hivi karibuni ya mawakili wawili zaidi wanaohudumia haki za binadam nchini Honduras yaliashiria hali ya hofu inayowakabili mawakili, waandishi wa habari na wateteaji wa haki za bindam nchini humo. Bi Pillay ametoa wito kwa serikali kuchukua hatua za dharura kukabiliana na hali ya kutoadhibu wanaotekeleza mauaji hayo, ambayo inaendeleza uhalifu kama huo.

Wakili Antonio Trejo-Cabrera, ambaye ni maarufu kwa kutetea makundi ya wakulima wadogowadogo katika eneo la Aguan nchini Honduras, aliuawa kwa kupigwa risasi mnamo siku ya Jumamosi.

Wakili huyo alikuwa amepokea vitisho vya kuuawa mara kwa mara miezi michache kabla ya kifo chake. Siku mbili baadaye,Manuel Díaz-Mazariegos, mwendeshaji mashtaka katika mji wa Choluteca, ambaye pia alihusika na kesi za haki za binadam, alipigwa risasi na kuuawa. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)