Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nyota wa Bollywood awa balozi wa hisani UM:UNAIDS

Nyota wa Bollywood awa balozi wa hisani UM:UNAIDS

Umoja wa Mataifa umemtangaza nyota wa filamu Bollywood na mlimbwende wa zamani wa India Aishwarya Rai Bachchan kuwa balozi wake wa hisani atayechukua jukumu la kukabiliana na kuenea kwa maambukizi ya virusi vya UKIMWI.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari,Michel Sidibé, ambaye ndiye Mkurugenzi Mtendaji wa mfuko wa Umoja wa Mataifa unaojishughulisha na UKIMWI UNAIDS, amesema kuwa balozi huyo wa hosani anatazamiwa kuleta msukumo mpya kwenye mapambano ya UKIMWI.

Mwenyewe alikitaja kitendo cha kupewa balozi wa hisani kama heshimu na akahaidi kuweka ushirikiano wake wa dhati.

Alihaidi kuendelea kuziunga mkono juhudi za kukabiliana na tatizo la kusambaa kwa virusi vya UKIMWI na akaongeza kutumia uwezo wake kushagihisha kampeni za UKIMWI