Pillay ashangazwa na hukumu kali walizopewa waandishi watatu wa habari nchini Vietnam

25 Septemba 2012

Kamishina mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi pillay ameelezea mshangao wake kutokana na hukumu kali zilizotolewa kwa waandishi watatu maarufu raia wa Vietnam akisema kuwa hii ni dalili ya kutokuwepo uhuuu wa kujieleza nchini Vietnam hasa kwa wanaotumia mtandao kutoa malalamishi yao. Mnamo siku ya Jumatatu juma hili Bwana Nguyen Van Hai alihukumiwa kifungo cha miaka 12 gerezani naye Bi Ta Phong Tan akahukumiwa kifungo cha miaka 10 gerezani huku bwana Pan Thanh Hai akipewa kifungo cha miaka mitatu.

Wote hao walihukumiwa kwa kueneza propaganda dhidi ya taifa kwa kuweka makala kwenye mtandao kuhusu klabu ya wanahabari huru ambapo wao ni wanachama wakuu. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter