Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi zaidi kutoka Sudan wahamia Sudan Kusini:UNHCR

Wakimbizi zaidi kutoka Sudan wahamia Sudan Kusini:UNHCR

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa mashambulizi mapya ya angani na ardhini kwenye jimbo la Kordofan Kusini yanasababisha watu zaidi kuhama jimbo hilo wakielekea nchini Sudan kusini. Karibu wakimbizi 100 wanawasili kwenye mpaka kila siku kwenye mji wa Yida wengine wakiwa na afya duni na bila chochote. UNHCR inasema kuwa baadhi ya wakimibzi wanasema kuwa kati ya sababu zilizosababisha wao kukimbia ni pamoja ukosefu wa chakula kwenye jimbo la Kordofan Kusini. Kambi ya wakimbizi mjini Yida kwa sasa inawahifadhi wakimbi 64,200 ambapo UNHCR inasema kuwa idadi hiyo huenda ikaongezeka hadi wakimbizi 80,000 ifikapo mwishoni mwa mwaka huu ikiwa mapigano yataendelea. Melissa Fleming kutoka UNHCR anasema kuwa baadhi ya wakimbizi walivuka mpaka na silaha hatua ambayo inatishia usalama kwenye kambi.

(SAUTI YA MELISSA FLEMING)