Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lamchagua Mserbia kama rais wake

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lamchagua Mserbia kama rais wake

Baada ya kutangazwa kama rais mpya wa Baraza Kuu la 67 la Umoja wa Mataifa, Bwana Vu Jeremic ambaye ni raia wa Serbia, amesema kuwa mwisho wa kipindi cha uchungu kwa taifa lake umewadia.

Bwana Jeremic, ambaye ni waziri wa zamani wa mambo ya nchi za kigeni wa Serbia, amesema kuwa muhula wake kama rais wa Baraza Kuu utakuwa mwanzo wa kutambulika tena taifa lake kwenye jukwaa la kimataifa, kwani liliachwa nje kwa sababu ya vita.

Bwana Jeremic ambaye ni Mserbia wa kwanza kuongoza Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, amesema katika mahojiano na Ari Gaitanis wa Umoja wa Mataifa ya kwamba katika miezi 12 ijayo, ataangazia uendelezaji wa kusuluhisha mizozo kwa njia ya amani.