Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanaondesha ghasia dhidi ya wapalestina waendelea kukwepa sheria nchini Israel

Wanaondesha ghasia dhidi ya wapalestina waendelea kukwepa sheria nchini Israel

Taifa la Israel limeshindwa kuwachukulia hatua walowezi wa kiyahudi na wanajeshi wanaondesha ghasia dhidi ya Wapalestina na mali zao imesema ripoti kutoka kwa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa (OHCHR). Ripoti hiyo inasema kuwa kesi ya mwanajeshi wa Israel ya kumuua mwanammke wa kipalestina pamoja na mtoto wake bado imekwama huku vijana watatu ambao walishambuilia familia moja ya kipalestina na bomu la petroli wakipewa kifungo cha nyumbani baada ya siku tano.

Kati ya masuala yaliyotajwa kwenye ripoti hiyo ni pamoja na uharibifu wa mashamba ya misabibu na walowezi wa kiyahudi. Naibu kamishina mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Kyung-wah Kang anasema kuwa karibu miti 500 ya misabibu imeharibiwa tangu mwezi Agosti mwaka huu hatua ambayo imewapokonya wapalestina tegemeo lao.

(SAUTI YA KYUNG-WAH KANG)