Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban aitaka jamii ya kimataifa kuunga mkono utawala wa Palestina

Ban aitaka jamii ya kimataifa kuunga mkono utawala wa Palestina

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon ameitaka jamii ya kimataifa kuunga mkono zaidi utawala wa Palestina akisisitiza kuwa ikiwa hilo halifanyika basi huenda kukawa na misukosuko eneo la mashariki ya kati. Ban amesema kuwa kuwepo kwa mataifa mawili na mafanikio ya utawala wa palestina ndiyo masuala kuu ya kuleta udhabiti na maendeleo. Masuala haya ni lazima yalindwe na kutekelezwa kwa ukamilifu haraka iwezekanavyoa, amesema Ban. Ameongeza kuwa kushindwa kufanya hivyo sasa hivi, huenda kukatokea athari ambazo huenda zikaleta misukosuko. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)