Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamati ya uhamiaji juu ya Pembe ya Afrika na Yemen kukutana Djibouti

Kamati ya uhamiaji juu ya Pembe ya Afrika na Yemen kukutana Djibouti

Wataalamu wanaunda kamati ya pamoja kushughulikia uhamiaji katika eneo la Pembe ya Afrika na Yemen wanatazamiwa kuwa na mkutano wao wa pili huko Djibouti kujadilia namna pande hizo zinavyoweza kuimarisha mashirikiano kukabiliana na tatizo la uhamiaji.

Mkutano huo ambao umepangwa kufanyika kuanzia Septemba 23 hadi 24 mwaka huu unatazamia kuzileta pamoja nchi za Ethiopia, Somaliland, Puntland na Yemen.

Wajumbe kutoka Misri, Eritreia, na Saudia Arabia watahudhuria mkutano huo kama waangalizi wa kawaida.

Pamoja na mambo mengine mkutano huo unashabaha ya kukusanya nguvu za pamoja na kupitia mipango ambayo itaziwezesha serikali za eneo hilo kuwa na mashirikiano ya karibu ili kukabiliana na tatizo la uhamiaji.