IOM yaanza kuwatawanya wakimbizi walioko Doro ili kukwepa athari za mafuriko

21 Septemba 2012

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM limeanza kuwatawanya katika maeneo salama wakimbizi waliopiga kambi huko Doro Sudan Kusin kufuatia mafuriko yaliyolikumba eneo hilo ambayo yamavuruga shughuli za usambazaji wa misaada ya kiutu.

Pamoja na hatua hiyo shirika hilo limeweka zingatio kwenye maeneo ya afya na linasambaza maji safi na salama kwa wakimbizi zaidi ya 42,000 ili kuepusha uwezekano wa kujitokeza kwa magonjwa ya mlipuko.

Kambi hiyo ni sehemu ya kambi nyingine tano zilizoanzishwa kwa ajili ya kuwahifadhi zaidi ya wakimbizi 106,000 waliokimb ia machafuko katika jimbo la Blue Nile nchini Sudan.

IOM ambayo inatekeleza ombi la shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR inasambaza huduma mbalimbali ikiwemo maji safi na salama. Mvua kubwa iliyonyesha mapema wiki hii ilisababisha mafuriko makubwa yaliyosambaa kuanzia kambi ya Doro hadi maeneo ya jirani ya Bunj

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter