Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yahofia ongezeko kubwa la wakimbizi mashariki mwa DRC

WFP yahofia ongezeko kubwa la wakimbizi mashariki mwa DRC

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, leo limeelezea hofu yake kuhusu kuongezeka idadi ya watu walolazimika kuhama makwao mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, na ambao wanahitaji misaada ya kibindam, ikiwemo chakula.

Mapigano yameongezeka mashariki mwa Kongo, huku makundi ya wanamgambo yakipigania kupanua maeneo ya umiliki na mamlaka yao.

Mapigano hayo, pamoja na ukiukaji wa haki za binadam, ukiwemo mauaji, uporaji mali, ubakaji na utekaji nyara, yamesababisha watu wengi kuhama kutoka mikoa ya Kivu Kaskazini na Kusini, Katanga Kaskazini, Maniema na Orientale. Shirika la WFP lilitoa msaada kwa wakimbizi 730, 000 ndani mwa Kongo, wanaoishi kambini, makazi ya dharura au familia zingine.

Elizabeth Brys kutoka WFP amesema kwa sababu ya idadi kubwa ya wakimbizi wapya, WFP inaomba msaada zaidi wa ufadhili.

(ELISABETH BRYS)