Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Balozi Mahiga alaani shambulizi la bomu mjini Mogadishu

Balozi Mahiga alaani shambulizi la bomu mjini Mogadishu

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Somalia, Augustine Mahiga, leo amelaani vikali shamulizi la bomu lililofanywa kwenye mkahawa mmoja maarufu mjini Mogasishu, na kutoa wito hatua za amani na utulivu zilizopigwa nchini humo zibaki kwenye mkondo wa kwenda mbele.

Katika taarifa yake kufuatia shambulizi hilo, Bwana Mahiga ameshangazwa na kukilaani kitendo hicho, ambacho amekitaja kama cha uoga na kisichokuwa na maana yoyote. Ameongeza kuwa vitendo kama hivyo vinaweza tu kuchagiza kujitolea kwa watu wa Somalia kukataa ghasia na kuendelea kutafuta suluhu ya amani kwa mzozo uliopo. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)