Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ofisi ya haki za binadamu yalaani mateso kwenye gereza nchini Georgia

Ofisi ya haki za binadamu yalaani mateso kwenye gereza nchini Georgia

Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesema kuwa ameshtushwa na kanda ya video inayoonyesha wafungwa wanaoteswa gerezani nchini Georgia. Pillay amesena kuwa taifa la Georgia ambalo limetia sahihi mkataba wa kupinga mateso linajukumu la kuhakikisha kuwa wafungwa hawapitii mateso na dhuluma zingine wakiwa kizuizini.

Amelaani vitendo vya mateso vilivyotekelezwa kwa wafungwa kwenye gereza hilo na kuonyeshwa kupitia karibu kanda nne za video zilizoonyeshwa kwa umma juma hili. Ametoa wito kwa serikali kuhakikisha kuwa madai hayo yote ya ukiukaji wa haki za binadamu na sio tu wale walioonyeshwa kwenye video hizo yamechunguzwa na wahusika kufikishwa mbele ya sheria.