UNHCR yawaandikisha shuleni watoto wakimbizi kutoka Lebanon

21 Septemba 2012

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR na washirika wanaendelea na programu ya kuwasaidia watoto wakimbizi 15,000 kutoka Syria kuijunga na shule nchini Lebanon. Kwa muda wa majuma mawili yaliyopita watoto 1,608 wamejiunga na shule za umma kaskazini na mashariki mwa Lebanon idadi hiyo ikiwa ni mara mbili zaidi ya idadi ya watoto wakimbizi waliojiunga na shule za umma mwaka uliopita. Nchini Iran uandikishaji wa watoto kwa muhula mpya shuleni unaendelea.

Kamati moja ya wakimbizi kwenye kambi ya Domiz karibu na Dohuk kaskazini mwa Iraq imeenda nyumba hadi nyumba kuwajulisha watu kuhusu kujiandikisha huku. Kwenye kambi ya Al Qaem watoto watapewa mafunzo kwenye mahema saba yaliyowekwa na la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter