Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watafuta hifadhi si wahalifu:UNHCR

Watafuta hifadhi si wahalifu:UNHCR

Shirika hilo la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa linasema kuwa watu wanaovuka mipaka ya kimataifa wakitafuta hifadhi hawastahili kuchukuliwa kama wahalifu na kufungwa. Shirika hilo linasema kuwa kukamatwa na kufungwa kwa wanaotafuta hifadhi na wale wanaokimbilia usalama wao ni kinyume na sheria za kimataifa.

Kulingana na maelekezo mapya yaliyotolewa hii leo UNHCR ni kuwa kuwafunga watafuta hifadhi ni hatua inayostahili kuwa ya mwisho huku UNHCR ikitaka kuchunguzwa kwa vituo vyote vinavyyowazuilia watafuta hifadhi. Alice Edwards ni afisa wa masuala ya sheria kwenye shirika la UNHCR.