Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wasomali waukimbia mji wa Kismayo

Wasomali waukimbia mji wa Kismayo

Zaidi ya watu 10,000 wameukumbia mji wa Kismayo nchini Somalia wakihofia oparesheni za kijeshi na makabiliano mapya limesema shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR. Ripoti kutoka Somalia zinasema kuwa wanajeshi wa muungano wa Afrika wanajiandaa kuuteka mji wa kismayo ambao umekuwa ngome kuu ya kundi la Al Shabaab.

UNHCR inasema kuwa hadi watu 7500 wamehama mji wa Kismayo kwa muda wa siku tatu zilizopita. Adrian Edwards kutoka UNHCR anasema kuwa wale wanaohama mji huo wana mipango wa kurudi mara hali itakapokuwa shwari.