Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa mawaziri wa UNECE waafikia kukabiliana na changamoto zinazoletwa na uzee

Mkutano wa mawaziri wa UNECE waafikia kukabiliana na changamoto zinazoletwa na uzee

Mkutano wa mawaziri kuhusu watu wanaozeeka umehitimishwa mjini Vienna, Austria, huku mawaziri hao wakiazimia kuhakikisha jamii ya watu wa umri wote kwa kuboresha hali ya maisha na namna ya kuzeeka. Mkutano huo umeandaliwa na Tume ya Kiuchumi ya Umoja wa Mataifa kuhusu bara Ulaya, na uliwaleta pamoja zaidi ya wahusika 500, wakiwemo mawaziri, maafisa wa ngazi za juu, wawakilishi wa mashirika yaso ya kiserikali na wanasayansi.

Azimio hilo la mawaziri linaorodhesha mielekeo ya kipaumbele katika awamu ya tatu, kati ya mwaka 2012na 2017, ya kutekelezwa mpango wa kuchukuwa hatua wa Madrid katika eneo ya UNECE.

Kwa kuangazia changamoto katika siku zijazo, mawaziri hao na wawakilishi wa kitaifa waliazimia kufikia malengo manne ya kipaumbele ifikapo mwaka 2017. Malengo hayo ni pamoja na kurefusha miaka ya kufanya kazi, kuchagiza uhusishwaji katika jamii na kutowabagua watu wazee, kuendeleza na kulinda heshima na utu, afya na uhuru wa watu wazee na kudumisha na kuendeleza ushirikiano miongoni mwa watu wenye umri unaotofautiana.