Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wakaribisha juhudi za Pakistan kukomesha visa vya watu kutoweka, ingawa bado kuna changamoto kubwa

UM wakaribisha juhudi za Pakistan kukomesha visa vya watu kutoweka, ingawa bado kuna changamoto kubwa

Kundi la wataalam wa Umoja wa Mataifa kuhusu watu kutoweka bila hiari, leo limekaribisha tangazo la serikali ya Pakistan kuwa itakabiliana na tatizo la watu kutoweka bila hiari, ingawa limetaja kuwa bado kuna changamoto kubwa.

Kundi hilo la wataalam limesema kuwa linatambua changamoto za kiusalama linalokumbaza nazo taifa la Pakistan, ingawa kwa mujibu wa azimio la mwaka 1992 kuhusu kuwalinda watu wote kutokana na kulazimishwa kutoweka, hakuna hali yoyote, iwe ya tishio la vita, vita vyenyewe, migogoro ya ndani ya kisiasa au hali nyingine yoyote ya dharura, inayoweza kutumiwa kama kisingizio cha kuwalazimu watu kutoweka.

Wamesema serikali ya Pakistan imekiri kuwa kumekuwepo utowekaji bila hiari, nab ado upo hata sasa. Lakini bado kuna utatanishi kuhusu idadi kamili na jinsi unavyotekelezwa. Wataalam hao wamekaribisha mchango wa vyombo vya sheria katika kuweka wazi tatizo hilo nchini Pakistan na katika kuwapata watu walotoweka. Wamesema jamaa za watu walotoweka wana haki ya kujua ukweli kuwahusu watu wao, na kupata haki kwa kuwachukulia hatua za kisheria wale waliotekeleza utowekaji huo.