Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM, Lebanon wahimiza haja ya kuwepo mashirikiano

UM, Lebanon wahimiza haja ya kuwepo mashirikiano

Mkuu wa vikosi vya ulinzi wa amani vya Umoja wa Mataifa nchini Lebanon amekutana na maafisa wa serikali kwa majadiliano yaliyolenga kuimarisha mashirikiano baina ya pande zote mbili.

Major-General Paolo Serra katika majadiliano hayo na maafisa wa serikali amezingatia maeneo ya ushirikiano baina ya vikosi vya ulinzi wa amani vya Umoja wa Mataifa na vikosi vya ulinzi vya Lebanon.

Pande zote mbili zimeelezea ulazima wa kuendeleza mashirikiano ya kijeshi kwa shabaha ya kudumisha hali ya usalama na amani.

Majadiliano hayo yamekuja katika wakati ambapo baraza la usalama wiki moja iliyopita lilipitisha azimio la kurefusha muda wa kusalia huko vikosi vya ulinzi vya Umoja wa Mataifa.