Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wajumbe wa UM nchini Iran wataka haki za kidini kuheshimiwa nchini Iran

Wajumbe wa UM nchini Iran wataka haki za kidini kuheshimiwa nchini Iran

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu nchini Iran Ahmed Shaheed na mjumbe kuhusu uhuru wa dini na imani Heiner Bielefeldt wamekaribisha kuachiliwa kwa mhubiri mmoja wa dini ya kikiristo aliyehukumiwa kifungo kutokana na makosa ya kuasi.

Wataalamu hao pia wameelezea hisia kutokana na hatua ya kuwakama na kuwazuiliwa wakiristo miaka ya hivi majuzi. Mhubiri huyo amekuwa kizuizini kwa muda wa miaka mitatu kutokana na mashtaka ambayo wajumbe hao wanasema kuwa hayawezi kuwa makosa kulingana na sheria za Iran. Kutokana na utafiti wa kibinafsi na kutoka kwa mashirika yasiyokuwa ya serikali bwana Shaheed anakadiria kuwa kuwa zaidi ya wakiristo 300 waliokamatwa na kufungwa kote nchini Iran tangu mwaka 2010. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)