WFP yaandaa mawasiliano ya mtandao kuhusu oparesheni zake nchini Syria

20 Septemba 2012

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP hii leo limewapa waandishi wa habari na watu wanaotumia mawasilino ya mtandao fursa ya kusikia oparesheni zake za misaada zinazondelea nchini Syria. Watumiaji wa mtandao na waandishi wa habari watauliza maswali ambayo yatajibiwa na Abeer Etefa ambaye ni msemaji wa WFP na afisa wa masuala ya mawasiliano eneo la mashariki ya kati na kanda ya kaskazini mwa Afrika.

Hivi sasa WFP inatoa msaada wa chakula wa dharura kwa karibu watu milioni moja wanaotabika ndani mwa Syria na ina mipango ya kuongeza idadi hiyo hadi watu milioni 1.5 mwezi unaokuja. Pia inawasaidia wale waliokimbilia mataifa jirani ya Syria yakiwemo Iraq , Jordan, Lebanon na Uturuki.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter