Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ugonjwa wa kipindupindu wasambaa nchini Sierra Leone

Ugonjwa wa kipindupindu wasambaa nchini Sierra Leone

Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa ugonjwa wa kipindupindu unaendelea kusambaa nchini Sierra Leone huku visa 19,000 vikiripotiwa. Hadi sasa ugonjwa huo umesababisha vifo vya watu 273. WHO inasema kuwa wilaya 12 kati ya wilaya 13 nchini humo kwa sasa zinaripoti visa vya ugonjwa huo ukiwemo mji mkuu Freetown.

Kusambaa kwa ugonjwa huo kunachochewa na hali duni za usafi na uhaba wa maji safi hasa kwenye mji mkuu Freetown. Dr William Perea kutoka WHO anasema kuwa miundo msingi duni pia huwa inawazuia watoa huduma za afya kayafikia kati ya maeneo yaliyoathirika zaidi vijijini.