Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mikakati ya kuchukua hatua inasaidia kukomesha matumizi ya watoto katika vita vya Silaha:UM

Mikakati ya kuchukua hatua inasaidia kukomesha matumizi ya watoto katika vita vya Silaha:UM

Zaidi ya mikakati 20 ya kuchukua hatua kukomesha matumizi ya watoto katika vita imeidhinishwa kote duniani.

Hii ndiyo taarifa iliyotolewa kwa Baraza la Usalama leo Jumatano na mwakilishi maalum wa UM kwa ajili watoto na vita vya silaha, Leila Zerrougui.

Amesema mipango ya utekelezaji sio tu mchakato bali ni chombo cha kipekee kilichoidhinishwa na baraza hilo kuzifanya nchi wanachama kufuata mwelekeo wake na kukomesha uhalifu dhidi ya watoto.

“Mwaka wa 2011 mipango ya kuchukua hatua ilitiwa saini nchini Afghanistan, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Chad, na mwaka huu Sudan Kusini, Myanmar na Somalia, ambako TFG ilitia saini Agosti, mkakati wa kwanza wa kuchukua hatua dhidi ya mauaji na ubakaji wa watoto. Hadi sasa mikakati 20 ya utekelezaji imekamilika au iko katika harakati za kutekelezwa”.

Baraza la Usalama lilipitisha azimio linalolaani vikali uhalifu dhidi ya watoto, ikiwemo kuwatumia katika jeshi, kwa mauaji, ubakaji na kwa kutekeleza mashambulizi dhidi ya shule na hospitali.