Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yaendesha juhudi kukabili mlipuko wa kipindupindu:Sierra Leone

WHO yaendesha juhudi kukabili mlipuko wa kipindupindu:Sierra Leone

Wataalamu kutoka shirika la afya ulimwenguni WHO wameanzisha juhudi kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu uliolipuka Sierra Leone.

Maafisa wa afya wanasema kuwa tangu kuzuka kwa ugonjwa huo tayari watu 271 wamefariki dunia na wengine wapatao 18,508 wameambukizwa.

Juhudi kubwa zinaelekwezwa kwenye maji ya kunywa ambayo inadaiwa kuwa ndiyo chanzo cha kulipuka ugonjwa huo.

WHO imeonya juu ya watu kutoingia nchini humo ama kuendesha biashara katika maeneo ambayo ugonjwa huo umeripotiwa kuwa katika kiwango cha juu.Wataalamu wa afya pamoja na kuimarisha mifumo ya utoaji matibabu lakini pia wanaendesha mihadhara ya wazi kwa ajili ya kuwajuzu wananchi namna wanavyoweza kuukwepa.