Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bahrain yaahidi kuboresha hali ya haki za binadamu

Bahrain yaahidi kuboresha hali ya haki za binadamu

Taifa la Bahrain limesema kuwa litawalipa fidia familia za waaandamanaji waliouawa wakati wa maandamano ya kuipinga serikali ya mwaka uliopita. Waziri wa mambo ya kigeni wa nchi hiyo Khalid Bin Ahmed Bin Mohamed Al Khalifa amesema kuwa fidia tayari zimelipwa kwa familia za watu 17 waliouawa za hadi dola milioni 2.6.

Akihutubia baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa Waziri huyo amesema kuwa mabadiliko ya sheria yanaendelea kwenye idara za mahakama kuhakikisha kuwepo kwa haki , kuzuia dhuluma na kulinda haki za wanawake na watoto. Amesema kuwa Bahrain imeitikia kutekeleza mapendekezo 158 kati ya mapendekezo 176 kutoka kwa baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa.

(SAUTI YA KHALID BIN AHMED BIN MOHAMED AL KHALIFA)