Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtaalam maalum wa UM kuhusu haki za watu wa asili azuru Namibia

Mtaalam maalum wa UM kuhusu haki za watu wa asili azuru Namibia

Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watu wa asili, James Anaya, anatazamiwa kufanya ziara Namibia tokea Septemba tarehe 20 hadi 28 ili kukagua hali ya watu wa asili katika taifa hilo.

Ziara hiyo ndio itakuwa ya kwanza ya aina yake kufanywa nchini Namibia na mtaalam maalum, ambaye amepewa jukumu la kuripoti kuhusu haki za watu wa asili na Baraza la Haki za Binadama la Umoja wa Mataifa. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)