Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama larefusha muda wa kusalia vikosi vya amani Liberia

Baraza la Usalama larefusha muda wa kusalia vikosi vya amani Liberia

Baraza la Usalama limerefusha muda wa kuwepo nchini Liberia vikosi vya ulinzi wa amani kwa kipindi cha mwaka mmoja zaidi, na limempa mamlaka Katibu Mkuu kupunguza kiwango cha askari katika awamu tatu.

Awamu ya kwanza inayotazamiwa kutekelezwa kati ya Octoba mwaka huu na Septamba mwakani, itawahusisha askari 1,900 watakaondolewa kwenye eneo hilo.

Wajumbe wa baraza hilo la usalama wakati wa upigaji kura walipitisha kwa kauli moja azimio la kutoa fursa kwa vikosi hivyo kuendelea kuunga mkono utendaji wa serikali ili kuimarisha hali ya usalama na amani.

Hivi karibuni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alipongeza utendaji kazi wa vikosi hivyo ambavyo vinaendesha mafunzo na kutoa utaalamu wa kisasa kwa kikosi cha polisi na maeneo mengine yanayohusika na usalama wa raia