Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwezi Agosti mwaka huu watajwa kuwa mwezi wa nane ulioandikisha viwango vya juu zaidi vya joto

Mwezi Agosti mwaka huu watajwa kuwa mwezi wa nane ulioandikisha viwango vya juu zaidi vya joto

Mwezi Agosti mwaka huu wa 2012 umekuwa mwezi wa nne ulio na kiwango cha juu zaidi cha joto tangu kuanza kunakiliwa kwa takwimu hizo mwaka 1880 kwa mujibu wa Shirika la kimataifa la utabiri wa hali ya hewa WMO. Mwezi wa Agosti pia unakuwa mwezi wa 36 na wa 330 wa kupanda kwa kiwango vya joto baada ya karne ya ishirini.

Sehemu nyingi za ulimwengu zilishuhudia viwango vya juu visivyo vya kawaida yakiwemo maeneo ya Kaskazini mwa Marekani, kati kati na kusini mwa Ulaya pamoja na eneo la mashariki na katikati mwa Asia. Hata hivyo maeneo ya Siberia yalishuhudia viwango vya chini vya joto.

Kwenye bahari ya Arctic kiwango cha barafu kilichaondishwa kilikuwa ni maili milioni 1.82 mraba kikiwa ndicho kiwango cha chini kwenye historia. Mwezi Agosti bahari ya Arctic ilipoteza tajkriban maili 35,000 mraba za barafu kila siku ambacho ndicho kiwango cha juu zaidi kuwai kushuhudiwa mwezi wa Agosti.