Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yatoa ombi la dola milioni 40 kusaidia watu waliohama makwao nchini DRC

UNHCR yatoa ombi la dola milioni 40 kusaidia watu waliohama makwao nchini DRC

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa hii leo limezindua ombi la dola milioni 40 za kuwasiadia karibu watu nusu milioni kwenye Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo waliolazimika kuhama makwao mashariki mwa nchi na kwenye nchi majirani zikiwemo Uganda na Rwanda.

Tangu kuanza kwa mapigano kwenye mkoa wa Kivu Kaskazini kati ya wanajeshi wa serikali na kundi la waasi la M23 mwezi Aprili takriban watu 390,000 wamelazimika kuhama ndani mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo hasa eneo la Mashariki na zaidi ya wengine 60,000 wamekimbilia mataifa jirani ya Rwanda na Uganda. Ikiwa mapigano yataendelea kwenye mikoa iliyo mashariki idadi ya wakimbizi wa ndani inatarajiwa kupanda hata hadi wakimbizi 760,000 miezi inayokuja. Melissa Fleming ni msemaji wa UNHCR.

(SAUTI  YA MELISSA FLEMING)