Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa wajumbe kutoka mataifa 124 duniani wakutana mjini Nairobi kujadili njia za usimamizi wa kemikali:UNEP

Mkutano wa wajumbe kutoka mataifa 124 duniani wakutana mjini Nairobi kujadili njia za usimamizi wa kemikali:UNEP

Zaidi ya wajumbe 500 na wataalamu kutoka mataifa 124 duniani, mashirika ya kimataifa, serikali, mashirika yasiyokuwa ya serikali na sekta za kemikali wanakutana mjini Nairobi Kenya kwa mkutano wa siku tano ambao unajadili njia za kukabiliana na athari za kemikali duniani.

Huku asilimia kubwa ya kemilikali zikiwa sasa zinatengezwa kwenye mataifa yanayoendelea na kutokuwepo njia mwafaka za kuweza kubaini athari za kemikali hizo kwa afya ya binadamu na mazingira, mkutano huu utajaribu kutafuta njia za usimamizi wa kemikali hizi.

Wajumbe hao wanesema kuwa hata kama kemikali zinatumiwa kwa wingi kila siku bado watu wengi hawaelewi athari za kemikali hizo na jinsi ambayo wanaweza kujikinga kutokana na madhara yanayosabishwa na kemikali.David Kampindula ni kutoka baraza la mazingira nchini Zambia na mmoja wa wajumbe kwenye mkutano huo.

(SAUTI YA DAVID KAPINDULA)