Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wapongeza zoezi la “kuwachangamanisha” wahamiaji wa Iran walioko Iraq

UM wapongeza zoezi la “kuwachangamanisha” wahamiaji wa Iran walioko Iraq

Umoja wa Mataifa umekaribisha kwa matumaini hatua iliyoanza kuchukuliwa na Iraq ambayo imewapangia kwenye maeneo mapya wahamiaji wa Iran waliokuwa wakiishi kwenye kambi moja iliyopo pembezoni mwa mji mkuu Baghdad.

Umoja huo wa Mataifa umesema kuwa zoezi la kuwawekwa kwenye maeneo mapya wahamiaji hao ni hatua ya kutia matumaini ambayo imeonyesha namna wananchi wa taifa hilo wa

Raia hao waliokimbia kutoka Iran walihifadhiwa kwa muda katika kambi moja Asharaf lakini hivi karibuni serikali ya Iraq ilitangaza kuifunga kambi hiyo kufuatia makubaliano yaliyofikiwa baina ya pande zote mbili, Umoja wa Mataifa na maafisa wa serikali.

Wahamiaji hao sasa wanachangamanishwa na raia wengine wa kawaida wa Iraq tayari kwa kuanza maisha katika mazingira ya kawaida.